Breaking News

Watu saba wafariki dunia kwa ajali Kigoma



Watu 7 wamefariki katika ajali iliyohusisha gari aina ya Scania Lori iliyotokea katika kijiji cha Mkongoro mkoani Kigoma.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa dereva wa lori hilo kushindwa kulimudu gari wakati akishuka kwenye mteremko uliokuwa na kona kali, na kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu hao saba.

No comments