Breaking News

Redio mazingira fm hivi karibuni itaanza kuwafikia wakazi wa vjijini kwa kuboresha usikivu wake.


Katika kuboresha huduma ya  matangazo, Redio MAZINGRA Fm, iliyoko Bunda Mkoani Mara imejizatiti kwa kuboresha miundombinu kama ujenzi wa mnara ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi walioko vijijini ambao kwa kiasi kikubwa hawafikiwi na huduma hiyo kwa ufanisi.

Hivi karibuni wafadhili wa miradi ya Redio hiyo ya kijamii kutoka Nchini Uholanzi bwana Jeroen Middelbeek pamoja na Bas Verzijden wamewaeleza wafanyakazi na uongozi wa redio hiyo kwamba wataendelea kuboresha miundombinu katika kituo hicho  ili adhima ya kuelimisha jamii ifikiwe kwa ufanisi hasa vijijini.

kwa upande wa uongozi wa redio mazingira fm, Kaim Mkurugenzi bwana Ally Nyamkinda amesema wafadhili hao wako tayari kusaidia miradi mbalimbali kituoni hapo lakini itafanikiwa kama kutakuwepo na nguvu ya pamoja baina ya wafanyakazi,serikali pamojana jamii kiujumla.

Hata hivyo meneja vipindi wa kituo hicho Bwana Gharos Riwa amewapongeza wafadhilihao kwa kukifanya kituo cha redio mazingira fm kuaminika na jamii kutokana na jitihada walizozifanya za kuwajengea mnara wenye urefu wa mita hamsini kwenda juu,kuwaletea majenereta matatu pamoja na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.




No comments