Breaking News

Kikundi cha pewa hundi ya milioni nne siku ya wanawake duniani-Bunda Mara

Kikundi cha Maisha Kinamama  kilichopo katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara kimepewa mkopo wa hundi ya shilingi milioni nne ikiwa ni njia ya kumkomboa mwanamke kiuchumi.
Akikabidhi hundi  mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi Jannet Mayanja kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyo fanyika kwenye viwanja vya Guta amewataka wanakikundi hao kutumia pesa hizo kwa malengo ili waweze kuondokana na hali tegemezi.
Pamoja na hayo Bi Mayanja amewataka wananchi wote  kuungana na kushirikiana kwa pamoja katika kuzuia na  kutatua vitendo  vya kikatili vinavyofanywa kwa wanawake   pamoja na  kuleta maendeleo kwa wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi  huku akiwaomba wanaume wote kuwaunga mkono wanawake kuhakikisha haki ya mwanamke inapatikana.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi afisa maendeleo  Stella Kazinja ametaja changamoto zinazokwamisha kumuwezesha mwanamke kiuchumi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia  kuwa ni  uelewa mdogo katika jamii kuhusu usawa wa kijinsia  ambapo swala hili limefanya mwanamke kutothaminiwa mchango wake katika mafanikio mengi ambayo yanapatika katika maeneo mbalimbali.
 
Kaulimbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni kuelekea uchumi wa viwanda,tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini.

No comments