RC Gambo amewataka wananchi kuwafichua wanaokwepa kod
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameitaka mamlaka ya mapato kushirikiana na wananchi kuwafichua wanaokwepa kulipa kodi.
Gambo ameyasema hayo wakati akizungumza katika wiki ya Elimu kwa mlipa
kodi iliyoenda sambamba na utoaji elimu kuhusu ulipaji kodi na faida
zake.
Amesema kuwa wananchi wana taarifa nyingi juu ya watu wachache ambao sio
waadilifu katika suala la kulipa kodi hivyo ameitaka tra kushirikiana
nao ili kuwafichua.
Mmoja wa wafanyabiashara Abduly Bale wanaomiliki mgahawa awashauri
mamlaka ya mapato kuwaangalia wafanya biashara wadogo wadogo ambao
huathiri wao kibiashara kwa kua hawana leseni wala kulipia mapato na
wao hulipia leseni pamoja na mapato .
Mwenyekiti wa chama cha Madalali wa Madini Arusha Jeremia Simoni
ameiomba mamlaka ya mapato kuwaangalia tajiri mwenye mali na mnunuzi
ndio wanaotakiwa kulipia mapato kwani wao hufanya biashara bila mtaji.
Meneja TRA mkoa wa Arusha Faustin Mdesa amesema mamlaka ya mapato
imekua na malengo ya kusisitiza utoaji wa risiti katika mauzo ya wafanya
biashara mfumo huo utawatunzia hesabu zao kua na uhakika wa mauzo yao.
Faustin amesema kuwa ulipaji kodi unapaswa kuwa utamaduni wa kila
mtanzania ili kuachana na kasumba ya kukwepa kodi inayorudisha nyuma
maendeleo ya nchi.
No comments