Hatimaye upelelezi kesi ya Aveva na Kaburu umekamilika.......Kesi Kuanza Kusikilizwa Aprili 5
Upelelezi
katika kesi ya utakatishaji fedha, dola za Marekani 300,000
inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey
Nyange, maarufu kama Kaburu, umekamilika na itaanza kusikilizwa Aprili 5
mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.
Katuga
aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa Aveva hayupo mahakamani hapo kwa kuwa
ni mgonjwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Baada
ya taarifa hiyo, Wakili anayewatetea washtakiwa hao,Steven Mwakibolwa
aliiambia Mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na kwamba hali ya Aveva
inaimarika ila siyo nzuri sana.
Hakimu
Simba, amesema kama hali ya Aveva itakuwa imetengemaa kesi hiyo
wataisikiliza mfululizo na kuongeza, kesi ilifunguliwa Juni 26, mwaka
jana na wajitahidi isikilizwe na kumalizika ndani ya miezi 12.
Washitakiwa
hao wanakabiliwa na mashitaka matano ya kutakatisha fedha na kughushi
ambayo wanadaiwa kuwa kati ya Machi 15 na Juni 29,mwaka 2016 Dar es
Salaam Aveva na Nyange kwa pamoja walikula njama ya kutakatisha fedha
kwa kupata Dola za Marekani 300,000 wakati wakijua ni zao la uhalifu.
No comments