Updates: Mbowe, Mwalimu Wameachiwa Kwa Dhamana......, Heche na Mnyika washikiliwa, Mdee na Matiko wanasakwa..
Viongozi
watatu wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana
huku wawili wakitakiwa kubaki.
Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.
Mwalimu
amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama
hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa
wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.
Heche
na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza
kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria
vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.
Dk
Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa
kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata
dharura.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
No comments