Breaking News

ZIARA YA MWENYEKITI UVCCM BUNDA YAENDELEA

Ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda *Ndg Gasper Charles* akiambatana na Katiba wa UVCCM Wilaya *Ndg Steven E. Shija* wameendelea na Ziara katika Kata tatu ambazo ni Nampindi, Igundu na Nansimo

Katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya alikutana na Mabaraza ya UVCCM Kata pamoja na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Taasisi za Serikali hususani Zahanati na Shule zilizopo ndani ya Kata hizo, pia aligawa Muhuri, Kanuni na Daftari maalumu kwa ajili ya kuandikia Kumbukumbu za Jumuiya Katika Kata zao

Katika Kutembelea Taasisi za Serikali na kuona Changamoto zinazowakabili aliwakumbusha Viongozi na Wanachama kuwa Mstari wa mbele kuhakikisha wanajiletea Maendeleo yao hususani Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na Matundu ya Vyoo katika Shule na Zahanati zinazokabiliwa na Changamoto hizo

"Maendeleo Shirikishi ndiyo Maendeleo endelevu, kila mmoja wetu anaowajibu wa kushiriki kwa kuchangia rasilimali wezeshi, Sisi Wanaccm tuwe wakwanza kuchangia na kuhamasisha na siyo wakwamishaji" Alisema Shija

Pia Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya aliwaonya Vijana kutojihusisha na Makundi yatakayoweza kukigawa Chama wakati wa Uchaguzi

"Ndugu Viongozi na Wanachama wenzangu, sihitaji kusikia au kuona mnajihusisha na makundi yanayohatarisha Uhai wa Chama chetu tutashughurikiana" alisema Gasper

Vilevile Viongozi walihimizwa kufanya Vikao kwa Mujibu wa Kanuni, kuingiza Wanachama wapya na Kuvaa Sare nyakati za Vikao vya Chama

Mwisho, Vijana walihimizwa kujikita kwenye Uzalishaji ili kuondokana na Utegemezi, na haya yanaweza kufanikiwa kwa kujiunga kwenye Vikundi ili Fedha zinazotengwa na Halmashauri kwa ajili ya Vijana ziweze kuwasaidia kuinua Uchumi wa Vijana wote

        *TUPO KAZINI*

*Imetolewa na :-*
*Ndg S.E.Shija*
*Katibu wa UVCCM Wilaya*
*Bunda, Mara*

No comments