Breaking News

FEDHA ZA JIMBO ZALETA UTOFAUTI WA HOJA MJINI BUNDA NI KATI YA MBUNGE NA DC

Siku chache baada ya Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Ester Amos Bulaya kuonya kuwa mtu akitaka kukosana nae aingilie fedha za jimbo hatimae Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwl Lydia Bupilipili ametoa wito Kwa kamati mbalimbali zinazoundwa kwa ajili ya maendeleo wilayani Bunda kuwa wasiingilie majukumu ya wataalam.

Bupilipili amesema kuwa amegundua kwamba zimeletwa fedha za serikali za mfuko wa Jimbo  mambo yameenda ndivyo sivyo.
''wataalam wako pembeni wanaosimamia huu mradi wa hizo fedha milioni 10 ni wengine, mlipaji mwingine''.

Na kiongeza kuwa ''mimi nafikiri hata kama ni vikao tunakaa kukubaliana tuwaachie wataalamu wawajibike kwenye nafasi zao bila tatizo lolote.'' alisema Bupilipili

Amesema waache kuingilia hata Kama hali ikoje lazima wataalamu watumie taratibu za kitaalam kuweza kuainisha ni nani akafanye nini na si kamati.
''ee sasa mnatengeneza kamati mnaenda mnasimama kwaniaba ya wataalam hatima yake unategemea ni nini alihoji,''alisema Bupilipili.

Na kuongeza kwamba ''halafu Hakuna fairness unakuta mtu amechukuliwa tu, anachkuliwa bila taratibu za tenda kufuatwa, mimi naona ni ukiukwaji mkubwa wa sheria kanuni na taratibu za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo''alisema DC

Hata hivyo kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Mh, Bulaya alisema kwamba mtu akitaka kukosana na yeye hizo pesa mtu aziguse,
''na ndiyo maana bunge lilipitisha sheria kwamba lazima msimamizi wa fedha za mfuko wa Jimbo awe mbunge, kwasababu mbunge wewe ndio utakuwa na uchungu na wananchi wako ukila utakuwa ni mbunge Mpumbavu sana" alisema Bulaya

Amesema mbunge akifanya dhili na fedha za wananchi wako utakuwa ni mpumbavu sana kwasababu kila mbunge anataka kuhakikisha maendeleo ya kweli kwenye Jimbo lake yanapatikana.

Amesema kwa upande wake hizo fedha zikiletwa anavyozipangilia ndivyo zinavyotumika.

Amesema hizo pesa zote zinapitishwa na bunge na ndiyo maana wamepewa mamlaka wanaozipitisha waje wazisimamie.

Swali Naomi yako ni yapi Katina hili ???

No comments