Breaking News

Timbulo awafungukia wanaoshobokea mali zake



Msanii wa BongoFleva anayetamba na kibao chake kipya cha 'Post', Timbulo amefunguka na kuwataka watu wasipagawe na vitu anavyokuwa anaviweka katika mitandao ya kijamii hasa hasa magari kwa madai sio ya kwake huwa anaazima ili apigie picha.

Timbulo amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya watu wengi kujiuliza maswali mengi kuwa anapata wapi jeuri ya kubadilisha magari ya kifahari kila uchao wakati haonekani hata kufanya 'show' msanii huyo.

"Mimi ni msanii tu, halafu yale magari watu wasipagawane nayo ninayoyaweka instagram, ni magari ya ma-boss wakina Chief Kiumbe. Kwa hiyo wasipagawe na kila wanachokiona ukurasa wangu wa kijamii maana vingine vinakuwaga ni ku-entertain tu, ndio maana hatupendi hata kuweka wazi magari ya watu", amesema Timbulo.

No comments