Breaking News

Imethibitika Korosho zenye kokoto nchini Vietnam zilitoka Tanzania



Serikali imethibitishiwa kuwa makontena mawili yaliyokutwa nchini Vietnam na korosho zilizochanganywa na kokoto zilitoka Tanzania.

Hayo yamethibitshwa leo Alhamisi, Machi 22 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo, Khasim Mbofu, wakati akikabidhi ripoti ya uchunguzi wa sakata hilo kwa serikali mkoani Dodoma.

Wakati tukio hilo linatokea, wananchi wengi walishangazwa na kitendo hicho huku wakidai, kawaida kila anayepeleka korosho ghalani kuuza lazima zimwagwe, zionekane au kuwe kuna ukaguzi kuhakikisha mzigo uko sawa.

Wengine walidai huenda kitendo hicho kikaathiri vikubwa uchumi wetu, kwa kujiharibia kwenye soko la dunia.

No comments