Breaking News

Waziri wa Nishati atoa agizo kwa Wakandarasi wa REA nchini



WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza wakala wa nishati vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanaunganisha umeme kwenye vijiji vitatu kila wiki ili kutoa fursa ya wananchi kufikiwa na huduma hiyo muhimu.

Dkt Kalemani aliyasema hayo jana wakati akizindua upatikanaji wa huduma ya umeme chini ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III) katika kijiji cha Magumbani kitongoji cha Mbuluni Kata ya Moa wilayani Mkinga mkoani Tanga.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba na uwashwaji wa huduma ya umeme katika Kijiji hicho ili kuwawezesha kupata huduma hiyo ilikuwa haipo awali katika eneo hilo,Alisema kwani hayo ndio malengo waliowapa ikiwa ni mpango mkakati wa kuha kikisha wanafikia malengo ya kuwapelekea umeme watanzania wote ifikapo mwaka 2021/2022 ili waweze kunufaika kupitia huduma hiyo .

“Leo tutaangalia mlipowasha lakini niwaagize wakandarasi tunataka kuona kila wiki vijiji vitatu vinawashwa umeme kwani wananchi wanauhitaji mkubwa wa kufikiwa na huduma hiyo hivyo hakikisheni hilo mnalitilia mkazo mkubwa “Alisema.

No comments