Breaking News

WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA OFISA ELIMU MJINI BUNDA.

PICHA NA MTANDAO. 
 
Wanafunzi katika shule ya msingi Balili B halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara wameandamana mapema leo  asubuhi 21.3.2018 hadi zilipo ofisi za Ofisa elimu Msingi mjini hapo baada ya mwenzao kugongwa kwa gari katika kivuko cha watembea kwa miguu kilichopo karibu na shule hiyo.

Tukio hilo la kugongwa kwa gari hadi kufa limempata Mwanafunzi  wa darasa la sita aitwae Julius Nyerere mwenye umri wa miaka 12 na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali teuli ya wilaya ya Bunda DDH.

Mashuhuda wa Tukio hilo wamesema wameshuhudia mwanafunzi huyo akigongwa  kwa gari lenye rangi ya Dark blue ambalo wao wamelihusisha na gari la askari mmoja wa jeshi la polisi waliemtaja kwa jina moja la afande Calvin.

Aidha alipouliza afisa mkaguzi wa jeshi la polisi afande Rose mbaga aliyefika katika eneola tukio kwamba askari wa jeshi la polisi ndiye aliyehusika na tukio hilo amesema kwamba si kweli na watu waliokuwa wanatoa maelezo hayo wamefikishwa polisi kushuhudia na kutonyeshwa magari yaliyopo kutamba gari lililohusika na ajali na kujiridhisha kwamba hakuna kati ya yote yaliyokuwepo kituoni hapo.

hata hivyo tukio hilo  limepelekea wakazi wa mji wa Bunda na hasa mtaa wa balili kufunga barabara ya Musoma -Mwanza kwa Muda kwa kuweka mawe na magogo barabarani kushinikiza serikali kutoa kauli kuhusu tukio hilo.

No comments