Breaking News

WALIMU WA KASKAZINI WANARUDI KWAO.

Baraza la Madiwani ya halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara wameshangazwa na hatua ya Baadhi ya Waalimu walioajiriwa wilayani hapo kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini hasa Kilimanjaro na Arusha kuhama na kurudi kwao na wengine pasipo kufuata utaratibu.

Hoja hiyo imeibuka katika baraza hilo baada ya Diwani wa kata ya Igundu Bwana Poul Nyamkinda kuhoji utaratibu unaotumka kuhamisha waalimu kwani wasiopugua 10 wamehama katika kata yake.

Naye diwani wa viti maalum Godriver Masamaki amesema miaka ya 2011,na 2012 waliletewa waalimu wengi kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Singida lakini hivi sasa wameamua kurudi kwao.

Alipoulizwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh, Isack Kabugu kuhusu nini kifanyike,amesema "kama wachaga wameamua kurudi kwao, basi nasi waalimu wanaofundisha Mikoa mingine warudi watufundishie watoto wetu".

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameaidi kukutana na katibu mkuu wizara ya elimu pamoja na Waziri wa tamisema kujadili suala hilo.

No comments