Breaking News

WAANDISHI KUTOKA REDIO ZA KIJAMII WATAKIWA KUJIKITA KATIKA KUANDIKA HABARI ZINAZOLENGA HAKI ZA KIBINA FFS AMU.

AweKatika kuelekea uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mitaa mwaka kesho2019 waandishi wa habari kutoka radio za kijamii nchini wamekumbushwa kutekeleza wajibu wao kwa kuandika habari zinazolenga haki za wananchi.

Hayo yamejiri katika semina ya siku moja mijini Dodoma iliyosimamiwa na Kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC.

Mwezeshaji wa semina hiyo Dr. James Jesse mwanashria na Mwalimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam amesema katika haki za binadamu miongoni mwa mambo yanayotakiwa kukumbushiwa serikali ni pamoja na mchakato wa katiba mpya ambayo mpaka sasa inamkwamo.

Amesema suala la katiba mpya limetumia muda mwingi na gharama kubwa lakini halikufika tamati ambapo ameshauri njia tatu zilizopendekezwa na wataalamu kulifanikisha.
Njia alizozisema ni kuendeleza mchakato mpya ilipoishia, kuitisha kwa mara nyingine bunge la Katiba,na kutumia kamati ya wataalam.

Aidha katika hatua hiyo waandishi wa habari wamepigia kura njia wanayoona ni rahisi kunasua suala la katiba mpya katika mkwamo huo ambapo kati ya waandishi  37, 13=35.1%, wameunga mkono kuendelea na katiba mpya ulipofikia,7=19%wamependekeza iitishwe bunge la katiba Mpya, na 17=45.9%
wameridhia kuundwa kwa kamati ya wataalam isiyoingiliwa kufanikisha mkwamo huo.

No comments