Breaking News

RAIS MAGUFULI AZINDUA BENKI YA CRDB TAWI LA CHATO.

Waziri wa nishati na mbunge wa Chato, Medard Kalemani ambae ameiomba benki ya CRDB iwasaidie ujenzi wa uwanja mkubwa wa Chato 'Chato stadium' pia amewaomba CRDB walipokuwa wawaachie ili waweke 'Chato habari news' au wawauzie kwa bei nafuu.

Kalemani anasema Chato ilikuwa kijiji kati ya vijiji na safari ya maendeleo ilianza mwaka 1995 Dr. Magufuli alipochaguliwa kuwa mbunge.

Anaeongea sasa ni mkurugenzi wa CRDB, Charles Kimei ambae anaanza kwa kuwashukuru wote waliohudhuria. Anasema safari ya benki ya CRDB mpaka inavyoonekana leo ni ndefu na haikuwa rahisi.

Anasema Rais Magufuli alimuomba afungue na yeye akamwambia Chato haina biashara ya kuweza kuhimili tawi, Naye Dr. Magufuli akamjibu 'No research, no right to speak' ana akasema atamuwezesha kufanya utafiti na vijana wa CRDB walienda na kutoa mrejesho kuwa panaendelea lakini bado, alipomwambia Dr. Magufuli akasema vijana wake hawana vigezo. Kimei anasema baadae ikaonekana ni kweli na Sacoss kisha tawi dogo vyote vilifanya vizuri.

Kimei anasema anaiomba bodi iridhie tawi liitwe JPM branch kwa sababu tawi hilo ni jitihada zake.

Kimei anasema CRDB ina amana ya trilioni 4.4 na hali hio inamaanisha vyuma vimelegea. Kimei pia amesema CRDB wanawaunganisha watu kutekeleza sera ya viwanda.

Anasema mikopo wanatoa kila mahali ikiwemo kwenye elimu. Kuhusu uwanja anasema hilo ni muafaka na wao hawajaondoka na wataangalia baada ya tathmini ili iwe stadium nzuri yenye hadhi ya benki.
-----
Rais Magufuli anakabidhiwa hundi yenye thamani ya milioni 50 kutoka kwa benki ya CRDB kwa ajili ya afya ambapo Kimei anasema kinachohitajika sasa hivi ni michezo, anasema siku zijazo wataidhamini timu ya Chato na anawaona wakakamavu na siku moja timu ya taifa inawezekana kutoka Chato.

Anasema kuhusu ofisi zilizoombwa na mbunge(Ofisi za zamani za CRDB Chato), watawapa kwa mkopo baada ya kukubaliana bei na anaamini wanaweza kulipa.

No comments