Breaking News

Azam uso kwa uso na Mbao leo

Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati AzamFc  kuvaana na MbaoFC ya Jijini Mwanza   baada ya kumalizana na Mwadui FC  ambapo wanalambalamba hao walitoka kifua mbele kwa kuifunga timu hiyo bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Timu hizo mbili zitapimana nguvu hapo kesho majira ya saa1 Usiku katika dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi. Ambapo kila timu zina presha ya kutaka kupata ushindi wa kuibuka na Alama 3 ili kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi.

Akizungumza na waandishi Wa Habari  Ofisa Habari AzamFc Jaffary Iddy  leo katika ofisi zao Mzizima Jijini Dar es salaam amesema kuwa kikosi tayari kipo kambini na kinaendelea na mazoezi.

"Kikosi kipo  kambini kinaendelea na mazoezi yake  katika kuelekea kwenye mchezo huo wa aina yake Ambapo kila timu inaitaji ushidi, tunaieshimu Timu ya Mbao iko vizuri na Ina kikosi kizuri lakini na sisi Tumejipanga vema kubakiza Alama 3 Nyumbani"amesema msemaji huyo  Jaffary.

Maganga amesema kuwa wataendelea kumkosa mchezaji wao Yakubu Mohammed  ambaye alipata majeraha pamoja na Kipa wao namba 1 Razack Abarola.

"Wachezaji Wote wako fiti ila tutaendelea kumkosa mchezaji wetu Yakubu Mohammed aliyepata majeraha katika mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho FA  Cup ambapo  tulicheza na timu ya  KMC pamoja na kipa wetu Razack Abarola anaemalizia  kutumikia adhabu ya kutoshiriki Mechi tatu" amesema Jaffary Maganga.

No comments