Aslay ampiga marufuku mama mtoto wake
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya ambaye kwa sasa ni gumzo kwenye mitaa ya bongo Aslay, amefunguka
kuhusu kumpiga marufuku mama mtoto wake, kufanya kazi aliyokuwa
akiifanya.
Aslay na mama mtoto wake Tessy Chocolate
Akizungumza
kwenye FNL ya East Africa Television, Aslay amesema mama mtoto wake
ambaye anafahamika kwa jina la Tessy, hawezi akaendelea kufanya kazi ya
aliyokuwa akifanya ya 'video vixen', kwani amempiga marufu na kila
alichokuwa akitafuta anampatia.
“Hawezi kuendelea mimi ndio nimesema hawezi kuendelea, sidhani kama sasa hivi anapenda tena kufanya, kwa sababu mara nyingi yupo na mtoto, na yeye mwenyewe kuna mambo yake anafanya kitu kinachomuingizia hela, kwa sababu kule alikuwa anatafuta hela sasa hivi hela anapata”, amesema Aslay.
Msanii huyo pia ameweka wazi kuhusu tetesi za kuachana na mama mtoto wake huyo, na kusema kwamba hajawahi kuachana wala kutengana naye.

No comments